LUBUMBASHY FC ITAPANDA DARAJA MSIMU UJAO – JASPER KAZUNGU

Klabu ya Lubumbasy FC inatapanda kutoka ligi ya kaunti hadi ligi ya mkoa msimu ujao baada ya kampeni ya mwaka huu kumalizika.

Hiyo ni kulingana na nahodha wa klabu hiyo Jasper Kazungu anasema kwamba baada yakutamatika kwa mzunguko wa kwanza wa msimu huu sasa wanapiga tizi za ziada ili kujiimarisha kipindi hiki cha likizo.

Amesema kwamba Lubumbasy iko na matumaini makubwa kupanda kulingana na msimamo wa jedwali katika chungu chao.

Rafiki Lubumbashy inacheza ligi ya kaunti ya kilifi kwa mara ya kwanza kabisa msimu huu kwani  ilikuwa inacheza ligi ya eneo bunge la magarini msimu uliopita na kutokana na kuibuka mabingwa katika ligi hiyo walipanda daraja hadi ligi ya kaunti ya kilifi.