LIGI YA MAGARINI KUNG’OA NANGA WIKENDI IJAYO

Ligi ya eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi itaanza rasmi wikendi ijayo kwenye msimu mpya wa mwaka 2022/2023.

Kulingana na uongozi wa fkf tawi la eneo bunge hilo vilabu zaidi ya 30 katika eneo la Gongoni tayari vimesajiliwa huku eneo la Marafa kikao cha mwisho kikifanyika leo kubaini vilabu vyote pamoja na ratiba ya msimu ikitarajiwa kupangwa kabla ya juma hili kutamatika.

Uhaba wa udhamini katika ligi hiyo unasalia kuwa changamoto kubwa kuendesha ligi  huku FKF ikiomba wahisani kujitokeza kudhamini mashindano hayo.

Akizungumza na tama la spoti kupitia njia ya simu  mchana wa leo, katibu mkuu wa shirikisho la soka fkf mwite Emmanuel kazungu ametoa wito kwa viongozi kuingilia kati ili kusaidia wachezaji kutimiza ndoto zao.