Mkufunzi wa klabu ya Bayer Leverkusen Xabi Alonso anatumai timu yake itakuwa na motisha hata zaidi kuwinda kombe lingine baada ya kushinda kihistoria kombe la Bundesliga. Bayer Lverkusen bado inawinda makombe matatu msimu huu na usiku wa leo watakuwa wanachuana na klabu ya West Ham kwenye Ligi ya Europa.
Kutokana na mechi ya raundi ya kwanza Leverkusen wanaongoza Westham kwa jumla ya mabao 2-0
Kwengine ni kuwa Jurgen Klopp anasema Liverpool bado wanaangazia kwa 100% Ligi ya Europa wanapoingia katika mkondo wa pili wa robo fainali huko Atalanta wakihitaji kupindua uongozi mkubwa wa mwenyeji wao.
Klabu ya Liverpool ilichapwakichapo cha mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Anfield katika mechi ya kwanza lakini Klopp alikataa kukubali kwamba wamefika mwisho, akisisitiza kwamba chochcote kinawezekana
Ikumbukwe kuwa Mjerumani huyo alisimamia urejeo wa Wekundu hao maarufu kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona mwaka wa 2019 baada ya pia kuchapwa 3-0 kwenye mkondo wa kwanza.

