JUNJU NDIO MABINGWA WA KOMBE LA GAVANA KILIFI

Kikosi cha soka kutoka wadi wa Junju kutoka eneo bunge la Kilifi Kusini ndio mabingwa wa makala ya kwanza ya soka la Governors Cup kwa upande wa wavulana.

Walishinda ubingwa huo jana katika uwanja wa chuo kikuu cha Pwani baada ya kuizidi maarifa timu ya wadi ya Sabaki kutoka eneo bunge la Magarini kwenye upigani wa matuta.

Dakika 90 mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1 na kupitia matuta Junju walisajili ushindi wa mabao 4-3.

Anderson Chome ni mkufunzi wa Junju na anasema waliwazidi Sabaki kila idara na mikwaju ya matuta ndio ilikuwa siri ya kuibuka mabingwa kwao.

Kwa upande wa kinadada mabingwa ni vipusa wa wadi ya Kaloleni walioibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wadi ya Sokoke.

Mabingwa kwa upande wa wavulana na wasichana walituzwa laki tano pesa taslimu za Kenya huku nafasi ya pili wakituzwa laki tatu nafasi ya tatu wakituzwa shilingi laki mbili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *