KLABU YA GUSII UNITED YAPEWA ALAMA KISA WENYEJI WAKOSA KUWEKA MAZINGIRA SALAMA

Klabu ya Gusii United ndio klabu ya hivi punde zaidi kupewa alama tatu na mabao mawili katika mechi ya National Super League baada ya kuwasilisha gari la ambulensi lililokosa vifaa vya kutosha kuweka mazingira kamili ya kiafya kwa wachezaji.

Haya yanajiri siku chache baada ya tukio kama hilo kutokea kwa klabu ya daraja la kwanza Malindi Progressive fc kutoka malindi ambapo mechi ilisitishwa na komishna wa mechi na alama tatu kupeanwa kwa klabu ya Balaji EPZ siku ya Jumapili.

Kwa sasa klabu ya Malindi Progressive imewasilisha lalama zao kwa maafisa wa fkf pamoja na ushahidi wote wakiomba hatua kuchukuliwa kwa komishna wa mechi hiyo.