Mwakilishi wa wadi ya Mkomani kaunti ya Lamu Shekhuna Abbas amesema kuna haja ya kuwa na muda maalumu wa maboti na pikipiki kuhudumu nyakati za usiku kisiwani Amu kwa sababu za kiusalama.
Abbas amesema iwapo Maboti na pikipiki hizo zitapigwa marufuku kuhudumu nyakati za usiku itakuwa bora zaidi ili kudhibiti visa ya ukosefu wa usalama katika kaunti hiyo.
Kwa mujibu wa Shekhuna Abbas vyombo hivyo vya usafiri vimekuwa vikitumiwa katika biashara haramu kama usafirishaji wa dawa za kulevya na pia wahalifu kutumia kutekeleza visa vya uhalifu.
SHEKHUNA ABBAS ASEMA KUNA HAJA YA KUWA NA MUDA MAALUMU WA MABOTI NA PIKIPIKI KUHUDUMU KISIWANI LAMU

