KISHADA YAPIGWA SHOKA NA FKF

Klabu ya Kishada imepewa adhabu na shirikisho la soka katika daraja la pili kitaifa, adhabu ya kutolewa alama tatu baada ya kususia kuendelea na mechi dhidi ya klabu ya Kamtonga kutoka kaunti ya Taita Taveta.

Kulingana na taarifa zilizofikia Tama la Spoti ni kwamba klabu ya Kishada walikataa kuendelea na mechi baada ya kamtonga kupewa penalty mara mbili mechi hiyo ilipokuwa inaendelea.

Kwa mujibu wa sheria za soka ni kwamba adhabu ya kutolewa alama tatu iliwafaa Kishada kwani hao ndio walisusia mechi hivyo kunyanganywa alama hizo.

Mwendo wa saa tisa mchana wa leo, klabu hiyo ya Kishada itakuwa inawakaribisha Furunzi FC katika uwanja wao wa nyumbani wa shule ya Upili ya wasichana ya Joho Girls katika kaunti ya Mombasa.