Waziri wa michezo Ababu Namwamba amethibitisha kuwa kaunti ya Kakamega kutoka mkoa wa Magharibi ndio itakuwa wenyeji wa mashindano ya kombe la mataifa bingwa afrika maarufu kama Chan huku uwanja wa Bukhungu ukiwa kati ya viwanja ambavyo vinatarajiwa kutumika.
Kwa sasa uwanja huo unafanyiwa ukarabati kwa ajili ya mashindano hayo makubwa ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwezi September mwaka huu na Ababu anasema kwamba iwapo uwanja huo hautaweza kustiri mashindano yote basi viwanja vilivyopo karibu kama vile vya kisumu vitakuwa vinatumika.
Wakati hayo yakijiri gavana wa kakamega anasema tayari wamezamia ukarabati wa uwanja huo ili kufikia viwango vya CAF angalau kuweza kuandaa mashindano hayo ya kimataifa.

