Kwenye tuzo za Ballon d’or ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo ni kwamba mashambuliaji wa Real Madrid pamoja na taifa la Ufaransa mwite Karim Benzema sasa ndiye mshindi wa tuzo ya Ballon d’or mwaka huu.
Anakuwa mfaransa wa tano katika historia ya soka kushinda tuzo hiyo yenye hadhi kwa mchezaji ambaye alifanya bora zaidi duniani katika kipindi cha msimu mmoja.
Ni tuzo ambazo zimekuwa zikiwashughudia nguli wa Ureno Christiano Ronaldo na mwenzake wa Argentina Leonel Messi kuzimiliki kwa kipindi cha muda mrefu lakini kwa msimu huu Ronaldo aliorodheshwa katika nafasi ya mwisho kwenye wachezaji bora wa mwaka wakati Messi hakuweko katika orodha hiyo.
Mchezaji wa Barcelona mwite Alexia Putellas ndio mshindi wa Ballon d’or kwa upande wa kina dada mwaka huu. Tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka inayojulikana na kama Gerd Mulla ilimwendea Robert Lewandoski ambaye pia anakipiga kunako klabu ya Barcelona.
Thibaut Courtois ndio kipa bora wa mwaka baada ya kuwa na kiwango kizuri katika klabu yake ya Real Madrid.
Kiungo wa Barcelona Gavi ameshinda tuzo ya mchezaji mchanga wa mwaka wakati mchezaji wa taifa la Senegal lakini pia Bayern Munich mwite Sadio Mane ambaye aliorodheshwa katika nafasi ya pili kwenye Ballon D’or akishinda tuzo ya Socrates, tuzo inayopewa mchezaji aliyefanya utu zaidi katika kipindi cha mwaka huo na hatimaye klabu ya Manchester City inayoongozwa na mkufunzi Pep Guardiola ikishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka wa 2021/2022

