Baadhi ya viongozi wa kamati la bunge la kaunti ya Kilifi wameanza mahojiano ya kuwapiga msasa walioteuliwa na gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro kuhudumu kwa wizara mbalimbali kaunti ya Kilifi.
Viongozi hao wanaongozwa na spika wa bunge la kaunti ya Kilifi ambaye pia ni mwenyekiti Teddy Mwambire kwenye kikao cha kuwapiga msasa mawaziri hao wateule.
Aidha shughuli hiyo inatarajiwa kukamilika kabla ya juma hili.
WALIOTEULIWA KUWA MAWAZIRI KAUNTI YA KILIFI WANAHOJIWA KWA SASA

