JUNIOR STARLETS IKO GUU MOJA NDANI YA KOMBE LA DUNIA

Timu ya Taifa ya kina dada isiyozidi umri wa Miaka Kumi na Saba Junior Starlets, wamebakisha mechi mbili tu Kufuzu tena kwenye michuano ya kombe la Dunia, wakijiandikishia Nafasi kwenye raundi ya mwisho baada ya Ushindi Wa Mabao matatu sufuri nyumbani dhidi ya Uganda hapa Jana.

Kikosi Hicho Cha Mildred Cheche kilionyesha Mchezo wa Kuvutia katika Uga wa Nyayo Hapo Jana, Magoli mawili ya Brenda Achieng na Moja La Patience Asiko, yalitosha Kuipa Starlets Ushindi huku Wakifikisha Ujumla Wa Magoli matano baada Ya Mikondo miwili.

Kufuatia Ushindi huo Junior starlets sasa wataekeana miadi na Cameroon kwenye Mechi ya Mikondo miwili, wakicheza Nyumbani tarehe kumi na nane mwezi ujao kabla Ya Kucheza Mechi ya Mkondo wa Pili ugenini siku saba baadae, mshindi kwenye Mechi hizi za Mikondo Miwili akijiandikishia nafasi kwenye mashindano ya Kombe la Dunia Huko Morocco.