Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Mombasa Peter Magiri amesema idadi ya wanafunzi ambao wanajiunga na masomo ya Sekondari Msingi katika kaunti hiyo imefikia asilimia 70.
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kielimu kwenye shule ya upili ya wasichana ya Mbaraki katika kaunti ya Mombasa, Magiri amesema masomo ya wanafunzi hao yanaendelea vyema japo kuna msongamano wa wanafunzi madarasani.
Magiri amesema baadhi ya Madarasa ya Sekondari Msingi yametengewa jumla ya wanafunzi 25 pekee kwa kila darasa japo tayari shule hiyo ya Mbaraki iko na wanafunzi zaidi ya 50 huku wanafunzi wengine wakipelekwa shuleni humo kwa Masomo ya Gredi ya Saba.
IDADI YA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA JSS KAUNTI YA MOMBASA YAFIKIA ASILIMIA 70

