HAMTASHIRIKI MASHINDANO MAKUBWA AFRIKA BILA WANAWAKE ZENU – CAF

Shirikisho la soka barani Afrika Caf limetangaza kwamba haitaruhusu klabu yoyote kushiriki katika mashindano ya shirikisho hilo bila kuwa na klabu ya kinadada inayoshiriki katika ligi inayotambulika katika taifa wanalotoka.

Taarifa hiyo sasa inaiweka Gor Mahia lakini pia klabu ya Tusker roho juu pamoja na kuwa na tumbo joto kwani klabu  hizo kwa sasa ziko katika nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi za kuingia katika mashindano ya Caf msimu ujao.

Hapa nchini Kenya katika ligi kuu ya fkf, ni klabu ya Mathare United, Ulinzi Stars pamoja na Vihiga Bullets ambao wanaklabu za kinadada zinazocheza ligi zinazotambuliwa na CAF.

Sharti la viwanja duni pia huenda likawa pigo kwani kwa sasa nchini hakuna viwanja vyenye hadhi ikizingatiwa kwamba CAF walitangaza kuwa kiwanja cha Nyayo lakini pia Kasarani haviko katika hali nzuri ya kuandaa mashindano makubwa hivyo iwapo kutapatikana klabu zitakazoingia katika mashindano ya CAF,  mechi hizo itabidi zikachezwe Uganda au Tanzania.