Klabu ya Gor Mahia imemwandikia kinara wa muunganno wa Azimio One Kenya Raila Odinga kumuomba kubatilisha ratiba ya mkutano wake katika uwanja wa Kamukunji jijini Nairobi siku ya jumapili wakihoji kwamba mkutano huo utagongana na ratiba ya mashemeji dabi .
Gor mahia wanatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya mahasimu wao wa jadi AFC leopards jumapili dimbani Nyayo, na kulingana na waraka uliochapishwa mitandanoni na kutiwa sahihi na katibu mkuu wa Gor Mahia Sam Ochola umemuomba Raila Odinga kuahirisha mkutano wake au kuandaa mkutano huo masaa mazuri ili mashabiki wa timu hizi mbili ambao pia baadhi ni wafuasi wa kiongozi huyo wapate muda kuhudhuria.
Wakati hayo yakijiri Gor Mahia ambao ni mabingwa mara 19 wa ligi kuu nchini wamesajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Talanta Fc katika mtanange uliochezwa dimbani Nyayo.
Benson Omala aliendelea kungaa katika mechi hiyo kwa kufunga bao lake la 10 msimu huu, huku John Macharia leo akiingiam kambani lakini pia Joshua Onyango akitikisa nyavu.
Matokeo hayo yanaifanya Gor Mahia inayoongozwa na mkufunzi Johnnathan Mckinstry kusalia na alama moja pekee kupanda kileleni mwa jedwali la ligi kuu, huku wakiwa na mechi moja kiporo.

