EVERTON YAKATWA ALAMA

Klabu ya Everton imepata pigo tena kutoka usimamizi wa ligi kuu nchini Uingereza la kupunguziwa alama mbili.

Hii ni baada ya mwezi November klabu hiyo ya Merseyside kupunguziwa alama 10 kabla ya ombi lao kubatilisha uamuzi huo hadi alama 6

Kwa sasa Everton imesalia na alama mbili pekee kuingia katika eneo hatari la kushuka daraja.

Kupunguziwa alama kunakuja baada ya klabu hiyo ya Merseyside Blue kupatikana na hatia ya kukiuka mashairti ya kifedha. Klabu hiyo kwa sasa iko na wiki mbili kwenda kortini kubatilisha maamuzi ya korti