DIANA CHEMTAI APIGWA MARUFUKU YA MIAKA 6

Bingwa wa mwaka jana wa mashindano ya Boston Marathon Diana Chemtai amepigwa marufuku ya kushiriki mashindano ya riadha baada ya kuwa mkenya wa hivi punde zaidi kupatikana na hatia ya kutumia dawa haramu za kusisimua misuli.

Kitengo kinachosimamia uadilifu wa wanariadha kimempa marufuku ya miaka sita kutoshiriki mashindano yoyote kutokana na kutofuata kanuni za taaluma hiyo ikiwemo hiyo ya matumizi ya dawa pamoja na kutumia vyeti bandia wakati wa usajili.

Diana Chemtai sasa anaungana na wanariadha wengine akiwemo Mark Otieno ambaye atatumikia adhabu ya miaka miwili ya kukaa nje kutokana marufuku, huku serikali ya Kenya ikisema inalenga kupiga vita vikali dhidi ya matumizi ya dawa hizo katika lengo la kusafisha jina la Kenya katika riadha.