Collins Injera mwanaraga nguli wa hapa nchini ,36, pamoja na nyota wa miaka ya 90 wa raga ya Fiji Sevens Noa Nadruku,55, wanalengwa kuekwa katika orodha ya mashujaa wa mchezo huo almaafufu kama RugbyTown Walk of Fame zoezi ambalo litafanyika hii leo.
Injera mchezaji lakini pia nahodha wa kikosi cha Kenya cha wachezaji saba kila upande Kenya, amekuwa nchini Fiji kwa ziara ya wiki moja kama balozi wa mashindano ya McDonald’s Fiji Coral Coast Sevens yatakayoanza rasmi kensho hadi siku ya jumamosi.
Ikumbukwe kwamba Injera alianzia raga yake katika shule ya upili ya Vihiga Boys, na atakuwa mmoja wa maafisa watakaowapa mafunzo watu wanaotaka kucheza raga katika mashindano hayo wiki hii, mashindano ambayo yanafanyika mara ya kwanza tangia mwaka 2020 kabla ya ujio wa maradhi ya virusi vya corona.

