MAAFISA WA CDF WANAOJIHUSISHA NA UFISADI WALAUMIWA KWA KUCHANGIA KWA WANAFUNZI KUKOSA MSAADA WA MASOMO

Mbunge wa Voi kaunti ya Taita Taveta Hamisi Chome amewataka maafisa wa hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge nchini CDF kukoma kujihusisha na visa vya ufisadi kwani unachangia kwa wanafunzi kukosa msaada wa masomo.
Hamisi Chome amesema atahakikisha hazina hiyo inafanya kazi kama inavyopaswa ili wanafunzi waweze kuendeleza masomo yao bila changamoto zozote.
Akizungumza kwenye kikao cha kukusanya maoni kuhusu miradi ambayo itatekelezwa na hazina hiyo mbunge Hamisi Chome amesema ni sharti watakaojihusisha na ufisadi wakabiliwe kwa mujibu wa sheria.
Aidha, kwa upande wa maafisa wa hizina hiyo wameahidi kutoa fedha hizo bila kumbagua mwanafunzi yeyote na kuwataka wazazi kuhakikisha wanatuma maombi ya basari wakti huu ambao shule bado hazijafunguliwa kwa muhula wa kwanza wa mwaka huu wa 2023.