BUNGE LA KAUNTI YA TAITA TAVETA LAADHIBU WAWAKILISHI WADI WAWILI KWA KUWAONDOA MAMLAKANI.
Kaimu Spika wa bunge la kaunti ya Taita Taveta Anselim Mwadime ametangaza viti vya wawakilishi wadi ya Mboghoni mjini Taveta na Wadi ya Rong’e mjini Mwatate kuwa wazi. Kulingana na Mwadime, wawakilishi wadi hao ambao ni Dorcus Mlughu na Khalifa Taraya, wamekosa kuhudhuria vikao vinane vya bunge, hivyo hawapaswi kuendelea kuwa wanachama wa bunge hilo […]



