WATU ZAIDI WABAINIKA KUENDELEZA IMANI POTOFU YA MUHUBIRI TATA PAUL MACKENZIE

Makaburi mengine manne yamepatikana katika kijiji cha Binzaro, kaunti ya Kilifi.

Matukio hayo yamezua taharuki huku polisi na wakazi wakihofia kuwa huenda wafuasi zaidi wa dhehebu potovu katika eneo hilo wamefariki.

Wizara ya usalama inasema kuwa imetibua kuenea kwa dhehebu hilo ambalo linakisiwa kuandamana na mafunzo ya itikadi kali kama ilivyoshuhudiwa katika msitu wa Shakahola miaka miwili iliyopita.

Mmoja wa wakaazi wa eneo hilo Simon Menza amedhibitisha kupata mwili uliotuopwa sawa na watu wengine wanaoendeleza mfungo katika msitu huo.

Kwa upande wake John Karama amesema kuwa walipokea taarifa za kuwepo kwa watu wanaoendeleza imani potofu ya mfungo wa kufa katika msitu huo kutoka kwa baadhi ya watu waliokuwa wakiomba msaada kwa wananchi hao.

Karama ameelezea uwezekano wa kuwepo kwa makaburi mengi zaidi katika eneo hilo