Baraza la kitaifa la vijana (NYC) liko huru kuandaa uchaguzi wake wa kitaifa ambao umekwama kwa muda mrefu.
Hii ni baada ya Bazara la Mawaziri siku ya Jumanne, kuidhinisha kutolewa kwa shilingi milioni 165, zinazohitajika ili kufanisha uchaguzi huo.
Waziri wa Masuala ya Vijana Salim Mvurya, amefichua kuwa hatimaye uchaguzi huo, ambao umekwama tangu mwaka 2012, unaweza kuandaliwa baada ya kuidhinishwa kwa bajeti ya uchaguzi.
Baraza la kitaifa la vijana lilibuniwa chini ya Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ICT mwaka 2009, na hupigania haki za vijana, ujuwumuishaji katika mipango ya maendeleo ya taifa.
NYC hujumuisha viongozi 22, wanaochaguliwa kikatiba na wanachama wake waliosajiliwa.

