Kuna umuhimu wa idara ya mahakama kuongezewa mgao wa fedha katika bajeti yake ya kila mwaka.
Haya ni kulingana na mbunge wa Jomvu kaunti ya Mombasa, Badi Twalib ambaye amesema kuongezwa kwa fedha hizo, kutasaidia idara ya mahakama kuboresha utendakazi wake kwa wananchi.
Twalib ameelezea kuwa ukosefu wa fedha za kutosha katika idara hiyo, husababisha kushuhudiwa kwa visa mbali mbali vya utovu wa maadili, katika utendakazi wa wafanyakazi wa idara ya mahakama.
Mbunge huyo aidha, amepongeza utendakazi wa jaji mkuu nchini Martha Koome, kwa kile anachosema amesaidia pakubwa katika kuboresha utendakazi wa idara hiyo kote nchini.

