BUNTHWANI WATERFRONT YAFAIDI WANAMICHEZO

Ufukwe wa Bunthwani Water Front katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi unazidi kuwafaidi wanamichezo wengi katika taifa hili hususan kwenye michezo ya ufukweni kama vile soka, voliball pamoja na riadha.

Mohamed Hafith ambaye ni meneja wa ufukwe huo akizungumza na Tama la Spoti kupitia njia ya simu amesema kuwa kuwa mwaka huu wanalenga kuwasilisha ombi la kutaka kuandaa mashidnao ya kimataifa ya michezo ya ufukweni kama njia moja ya kuvutia watalii katika gatuzi hili.

Vilevile amethitisha kuwa kutokana na uwezo wa kuandaa mashidano ya Olimpiki, mwaka huu wanaomba mashindano yanayopangwa kufanyika Mozambiique yaletwe nchini Kenya.

”Uwanja huu kwa sasa unaweza andaa mashindano ya Olimpiki kwa sababu NOCK imefanya hivyo hapo nyuma. Mwaka huu tunalenga kutuma ombi la kutaka mashindano ya kimataifa yaletwe hapa kwa sababu tumeskia huenda yakaenda Mozambique” Alisema Mohamed.

Uwanja huo umekuwa ukiandaa ligi za mashinani kama vile Beach soka za timu zinazotoka katika eneo bunge la Malindi, mashindano ambayo yameanza kuvutia wachezaji na mashabiki wengi.