Ligi kuu nchini Uingereza imetoa taarifa kuwa Anthony Tailor ndiye atakaye kuwa refa wa mechi ya mechi itakayokutanisha Liverpool dhidi ya Arsenal wikendi ijayo.
Arsenal ambayo ilipigwa bao 2-0 na Bournemouth katika Dimba la ugenini. Hata hivyo kiungo wa Kati raia wa Uingereza Declan Rice anatarajiwa kukosa mechi hiyo
Rice ataikosa mechi hiyo kutokana na kula kadi nyekundu wikendi ilopita.
Ni mechi itakayochezwa Jumapili katika uwanja wa Emirates. Kabla ya kichapo cha wikendi klabu ya Gunners haikuwa imepoteza mechi yoyote ya ligi kuu msimu huu chini ya kocha Mikel Arteta

