BENNI McCARTHY AANZA KAZI

Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya wanaume Benni McCarthy,  amekitaja Kikosi cha wachezaji ishirini na watano kitachosafiri kuelekea Abidjan Ivory Coast hapo kesho, Tayari kwa Mechi za Kufuzu kwa Kombe la Dunia la Mwaka Ujao dhidi ya Gambia.

Kikosi hicho ambacho kitazama dimbani siku ya Alhamisi Kinajumuisha Kipa wa Bandari Faruk Shikalo na Kipa Ian Otieno wa Tusker, mabeki Joseph Okumu wa Stade de reims ya Ufaransa, Brian Mandela Wa Afrika Kusini, kiungo wa yanga Duke Abuya, washambuliaji Elvis Rupia na Masud Juma pamoja na Nahodha Michael Olunga .

Kikosi hicho hakijapokelewa vizuri na baadhi ya washikadau wa soka hapa Nchini, kwa upande wao wakisema kwamba McCarthy aliwatema wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani.

Mkufunzi Benni alichukua majukumu hayo rasmi wiki mbili zilizopita baada ya kuchaguliwa kuwa kocha wa timumya taifa ya Kenya na shirikihso la soka la fkf pamoja na wizara ya michezo.