SAMBURU LIONS KUFANYA USAJILI MSIMU HUU

Naibu mkufunzi wa klabu ya Samburu Lions Samuel Omondi anasema kuwa analenga kufanya usajili ili kuimarisha kikosi chake ili kumaliza msimu huu katika kiwango bora.

Omondi anasema anapolenga sana kufanya usajili ni eneo la mashambulizi huku akisema tayari yuko na baadhi ya wachezaji ambao anajiandaa kuwaweka kwenye orodha ya kikosi chake.

Ameeleza matumaini makubwa kuwa kwenye ligi ya daraja la pili msimu ujao, samburu lions inalenga kupanda daraja akikiri kuwa msimu huu kwao ni vigumu kupanda kutokana na kuanza msimu vibaya.

”Tunalenga kufanya usajili msimu huu hasa katika mapengo ambayo tuko nayo kwa sasa. Niko na wachezaji tayari ambao niko na orodha itakayonifanya nisaidia.” Alisema Omondi