UWANJA WA MASHEMEJI DABI WABAINIKA

Baada ya Sintofahamu Nyingi kusaamba Kuhusu uwanja utakaokua mwenyeji wa Mechi Kubwa hapa Nchini, Hatimaye AFC Leopards ambao watakua wenyeji wamefanikiwa kuupata Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, kwa Ajili ya pambano la Mashemeji derby tarehe Moja Siku ya Jumapili, Dhidi ya Wapinani wao wa Jadi Gor mahia.

Awali mechi hiyo iliratibiwa Kupigwa katika Uwanja wa Kasarani,lakini hali yake ya sasa ilifanya Ingwe kutafata njia mbdala, kwani awali Uwanja huo ulikua umefungwa kwa Ajili ya ukarabati taifa Likijitayarisha kwa Michezo ya Chan, na bado haujakua tayari vifaa vya ujenzi vikisalia uwanjani.

Awali Kogalo waliibuka Washindi wa Mikondo yote miwili ya Mashemeji Derby, wakiwacharaza Ingwe magoli mawili sufuri kwenye Mechi ya Mkondo ya kwanza, na Goli Moja sufuri kwenye mechi ya Mkondo wa Pili.