Ngarambe nzito ya soka la kinadada Afrika inatarajiwa kufanyika nchini Tunisia, ambapo hii leo mwendo wa Saa Kumi na Mbili Jioni Harambee Starlets Watazama Ndimbani, tayari Kumenyana na Timu ya Taifa Ya Tunisia kwenye Mechi ya Mkondo wa Pili ya Kufuzu kwa Makala ya WAFCON ya mwaka Ujao.
Mechi ya Mkondo wa Kwanza Iliyopigwa Ugani Ulinzi Sports Complex Ijumaa Wiki Jana, Iliishia Kutoka Sare tasa na kuelekea Kwenye Mechi hii Starlets wanahitaji ushindi au angalau sare,ili waweze kufuzu kwenye hatua ya Mwisho ya Makundi.
Iwapo Starlets Itafuzu, basi itamenyana na Mshindi wa Mechi kati ya Niger na Gambia, na Ushindi kwenye mechi hio ya itawaandikishia nafasi kwenye michuano ya Bara ya WAFCON.

