Shirikisho la soka hapa Nchini FKF linapanga kumng’atua Beldine Odemba kama mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Kina dada Harambee starlets, kufuatia sare tasa dhidi ya Tunisia kwenye mechi ya mkondo Wa Kwanza ya kufuzu kwa Wafcon ya mwaka ujao iliyopigwa ugani Ulinzi sports complex.
Odemba alipokea cheche kutoka kwa mashabiki na wachanganuzi WA soka hapa Nchini kufuatia mbinu anazozitumia kuchagua kikosi chake, swali kuu likiwa mbona aliamua kumchezesha Mfungaji Bora Wa ligi kuu ya Tanzania Jentrix Shikanngwa kwenye dakika 90 ya mechi.
Starlets wapo Safarini kuelekea Tunisia tayari kwa mechi ya mkondo Wa pili siku ya Jumatano, mechi hii ikiwa ni lazima kwao washinde ili kusalia kwenye mashindano hayo.
Mkufunzi Wa Zamani Wa Vihiga Queens Alexander Alumirah akiibuka mstari Wa mbele kumrithi Odemba.

