SERIKALI YA KITAIFA YAONYWA DHIDI YA KUCHELEWESHA MGAO WA FEDHA KWA SHULE ZA UMMA.

Miungano ya walimu ya KUPPET na KNUT eneo la Pwani, imeitaka serikali ya Kitaifa kuharakisha shughuli za ugavi wa fedha za kufadhili masomo kwa wanufunzi wa taasisi za elimu za serikali.

Wakingumza katika kaunti ya Mombasa, kwenye kongamano na walimu, viongozi hao wakiongozwa na katibu mkuu wa KUPPET kaunti ya Mombasa, Lynette Kamadi, pamoja na Dan Aloo wa muungano wa KNUT, wameelezea kuathirika kwa shughuli za masomo kwenye shule za umma, wakati mgao wao unapocheleweshwa.

Katika taarifa yao kwa waandishi wa habari, wamesema kuwa huenda utendakazi wa walimu shuleni ukarahishishwa, iwapo watakuwa wakipokea mgao hitajika kwa wakati unaofaa.

Hata hivyo mkurugenzi wa elimu katika eneo hilo la Changamwe kaunti ya Mombasa, Fatma Omara amelalamikia suala la wanafunzi wengi kutumia mihadarati, hatua ambayo imechangia pakubwa wengi wao kupotoka kimaadili.