Muungano wa wamiliki wa hospitali na vituo vya afya vya kibinafsi, vinavyotoa huduma za matibabu kupitia bima ya afya ya SHA, umetilia shaka suala la serikali kuu, kukusanya fedha za kutosha kupitia bima hiyo, kama ilivyoratibiwa wakati bima hiyo ikianzishwa.
Kulingana na kiongozi wa muungano huo daktari Brian Lishenga, hatua hiyo imetokana na suala la wakenya wengi, kusisitizwa kujisajili kwenye bima hiyo ya SHA, ila hawajapewa ufahamu wa kina kuhusiana na ada hitajika za kila mwezi.
Lishenga vile vile amesema kuwa, baadhin ya wakenya sasa wamesusia kulipia ada hizo, baada yao kukosa huduma za matibabu hospitalini, licha yao kugharamika malipo ya SHA kila mwezi.
Vile vile Lishenga amesema kuwa hatua ya vituo vya afya vya kibinafsi kujitoa kwenye SHA, ni kuhakikisha kuwa serikali kuu inatimiza ahadi walizotoa kuhusiana na utendakazi wa SHA na kuhakikisha kuwa wasimamizi wa vituo hivyo, wanapata pesa za kuwasaidia kuendeleza shughuli za matibabu.

