Manchester United imefuzu kwenye Hatua ya raundi ya kumi na sita Bora Katika kombe La bara Europa, baada ya kuicharaza FCSB waliokua nyumbani magoli mawili sufuri, kinda Kobbie Mainoo akiuona wavu na kupeana asisti ya mabao hayo kwenye kipindi cha pili.
Vigogo wa Uturuki Galatasaray walimaliza Fomu yao ya kwenda Mechi saba Bila kufungwa, walipoangukia Kipigo cha magoli mawili kwa moja mikononi mwa Ajax, Victor Osimhen akiwapitia goli hilo la kufutia Machozi kwenye dakika za lala Salama katika Kipindi cha Pili.
Vijana wa Ange Postecoglou kwa Upande wao wamefuzu moja kwa moja kwenye hatua ya kumi na sita bora, baada ya ushindi mkubwa wa magoli matatu sufuri ugani Hotspurs Stadium dhidi ya Wa Swizi Elfsborg.
Baada ya mechi za mwisho za ligi Hiyo kupigwa hapo jana usiku, Timu saba sasa Zimefuzu moja kwa moja kwenye Hatua ya Kumi na sita Bora, zikijumuisha vigogo wa Ligi Lazio, Manchester United, Athletic Bilbao ya Uhispania, Olympique Lyon ya Ufaransa, Huku Upande wa Jose Mourinho Fenerbahce, As Roma, Fc porto Na Ajax zikisalia kwenye Hatua Ya makundi.

