SERIKALI YA KENYA KWANZA YAKOSOLEWA KWA KUKOSA UFAHAMU WA WAHUSIKA WA VISA VYA UTEKAJI NYARA.

Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa nchini Barrack Muluka, amekashifu vikali hatua ya serikali kudai kutokuwa na ufahamu kuhusiana na anayetekeleza visa vya utekaji nyara katika taifa hili.

Kulingana na Barrack, serikali ya Kenya Kwanza imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa wananchi wa taifa hili na hivyo inapaswa kujiuzulu.

Akizungumza hapa kaunti ya Kilifi, Barrack amesema kuwa jukumu kubwa la serikali, ni kuwahakikishia wananchi wake usalama wa kutosha.

Aidha, amekashifu suala viongozi wa serikali ya Kenya kwanza, kudai kuwa vijana wamekuwa wakitekwa nyara kutokana na ukosefu wa maadili.