Masaa machache baada ya klabu hiyo ya kaunti ya Kwale kuchangiwa na mashabiki kuheshimu ratiba dhidi ya klabu ya Dimba Patriots wamekubali kichapo cha mabao 2-1.
Chini ya masaa 24 yalopita klabu hiyo iliomba mchango kwa mashabiki kutokana na kulemewa na masuala ya usafiri jambo ambalo awali walitoa taarifa kuwa wangekosa kuheshimu ratiba.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Phelix Ogutu amevunja ukimya wake na kusema kuwa ukosefu wa udhamini katika timu hiyo ni jambo ambalo limeifanya klabu hiyo kushindwa hata kusajili wachezaji wazuri ili kuleta matokeo.
”Wacha niiweke wazi, hapa Assad kwa sasa kuna matatizo ya udhamini. Hali hii imenifanya hata kushindwa kusajili wachezaji wazuri wanaoweza kubeba timu.” alisema Ogutu
Ogutu amewaomba mashabiki kuwa na subra na timu hiyo huku akielekeza matumaini yake kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari akisema kuwa huenda wakasajili wachezaji ambao wataleta uzoefu na timu kuanza kusajili matokeo mazuri.

