MAREFA WANAHARIBU SOKA NSL

Maamuzi mabaya  ya marefa katika ligi za Kenya yanazidi kutajwa kuwa jambo linaloharibu soka la taifa hili. Wa hivi punde zaidi ni kocha mkuu wa klabu ya SS Assad Phelix Ogutu.

Kocha huyo mzoefu anadau kuwa marefa wanaoendesha ligi kubwa za Kenya kama ile ya kitaifa ya Super League wanakosa uhitimu Fulani kuchezesha ligi hizo jambo ambalo limeanza kupelekea viwango vya soka  kushuka.

Ametoa wito kwa shirika linalowapa kazi marefa KEFORA pamoja na shirikihso la soka FKF ili kutatua utata huo.

”Marefa wengi katika NSL hawaonyeshi uzoefu kabisa, ni jambo la kutiliwa shaka kwani hao ndio wanalemaza soka la kenya. FKF na KeFORA zinafaa zichukue hatua mara moja kukomboa soka la taifa hili”, Alisma Ogutu

Wakati hayo yakijiri klabu ya SS Assad mchana wa leo imetoa taarifa kuwa kesho haitasafiri kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Dimba Patriotes Ugenini.

Kati ya masuala ambayo yamechangia klabu hiyo isisafiri ni ukata wa kifedha jambo ambalo kulingana na taarifa ya klabu hiyo kupitia ukurasa wa facebook wameeleza kusikitika nazo na kuwaomba mashabiki radhi kwa kufeli kuwapa burudani la soka hiyo kesho .