MWALE TAYARI KUJIUNGA NA KLABU MPYA

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Junior FC Zablon Mwale anasema yuko tayari kujiunga na klabu ambayo itahitaji huduma zake. Ameyasema hayo baada ya kujiuzu kutoka wadhifa wakewa ukocha kwa klabu hiyo ya       Wundanyi inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili.

”Kwa sasa mimi sina klabu lakini klabu ikija ikisema inahitaji uduma zake mimi nitaangalia halafu nitaona kama nitasaini ama kutaendaje. Wajua mimi ni mwanasoka kwa hiyo siwezi kuachana na soka kabisa” Alisema Mwale

Mwale alijiuzulu mwanzo mwa wiki hii kwa kile alichojitaja kuwa amekuwa akikosewa heshima katika klabu hiyo.

Pia amewashauri wachezaji aliowaacha Junior FC kuzidi kujituma kwa ajili ya matokeo bora wanapoendelea na msimu huu.

Mwale ameachana na klabu hiyo ikiwa na alama kumi kwenye ligi baada ya wikendi kuizaba Malindi United bao 1-0 katika uwanja wao wa Nyumbani.