Klabu ya Liverpool Jumapili ilirefusha uongozi wao wa ligi na alama 9 baada ya kuinyuka klabu ya Manchester City kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wa Anfield.
Ni mechi ambayo ilimshuhudia mholanzi Cody Gakpo akiingia kambani kunako kipindi cha kwanza kabla ya Mohamed Salah kufunga bao la pili kupitia mkwaju wa tuta baada ya pale Luis Dias alipofanyiwa madhambi. Kwa sasa Mohamed Salah amefikisha mabao 11 pamoja na kutoa pasi za mabao 7 msimu huu akishindwa bao moja pekee na Erling Haaland wa Manchester City
Hii ilikuwa mechi ya nane mfululizo kwa kocha wa Machester City Pep Guardiola kushindwa kusajili ushindi wowote katika mashindano yote anayoshiriki msimu huu.
Kwa sasa Liverpool iko na alama 34 nyuma yao karibu ni Arsenal wenye alama 25 sawa na Chelsea wenye alama 25. Manchester City kwa sasa wameshuka hadi nafasi ya tano wakiwa na alama 23.
Msimu huu Liverpool imekuwa kwenye ubora katika mashindano makubwa hasa Uefa wakiwa kwa sasa kwenye kundi la pamoja wako na alama 15 bila kupoteza mchezo wowote. EPL wamepoteza meci moja pekee dhidi ya Nottingham Forest bao 1-0 na sare dhidi ya Arsenal majuma kadhaa yaliyopita.
Arne Slot ni kocha mpya wa Liverpool katika msimu wake wa kwanza akirithi mikoba kutoka kwa Jurgen Klopp akitokea Feynoord FC ya Uholanzi.

