Waziri wa michezo nchini Kenya Kipchumba Murkomen anasema serikali haitaendelea kumlipa kocha mkuu wa Harambee Stars Engin Firat baada ya kushindwa kuisaidia timu ya taifa ya soka Harambee Stars kufuzu katika mashidano ya AFCON mwaka ujao na badala yake atafutwa kazi.
Murkomen akizungumza hiyo jana katika jingo la Talanta Plaza jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa jopo kazi la kukagua na kurekebisha sheria ya michezo ya mwaka wa 2013 alieleza shinikizo anazopata kutoka kwa wakenya za kumpiga kalamu kocha huyo kwa kufeli kutimiza wajibu wake na kusema wakati sasa umefika kumtimua kwa kutumia sheria.
”Hatuna budi kutumia sheria zile zile na mkataba uliokuwa umewekwa hapo awali. Kati ya makubaliano ni kufuzu kwa AFCON na hilo halijafanyika. Kwa sababu sisi kama wizara ndio hulipa mshahara wa kocha huyu tumeamua kusitisha malipo.” Alisema Murkomen
Hata hivyo Murkomen amejitetea kwa kujiondolea lawama akisema serikali ya Kenya iliwajibika vilivyo kuisimamia timu kipindi hiki cha kutafuta tikiti ya kufuzu kwa afcon akisema kuwa, Harambee stars ilisaidiwa vya kutosha.

