Kuna umuhimu mkubwa wa viongozi waliochaguliwa wiki jana katika shirikihso la fkf tawi la kaunti ya kilifi kushirikiana kupeleka soka mbele. Ni kauli ya Collins Otieno Omol meneja wa timu ya Yanga kutoka mji wa Malindi klabu inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa.
Anasema kaunti ya Kilifi iko na talanta chungu nzima na iwapo watashikwa mkono, vijana wengi wanauwezo wa kutangaza soka la Kenya kimataifa.
Ameshauri kuwa talanta zilizopo mitaani kwa sasa hazifai kuachwa zikaharibika.
Wikendi ijayo siku ya jumapili Yanga inatarajiwa kusafiri hadi Mariakani kukipiga dhidi ya Mariakani Fc na Collo anasema ana matumaini makubwa wikendi hii Yanga itasajili matokeo bora baada ya wachezaji wengi kurejea katika timu hiyo baada ya mitihani ya kitaifa ya KCSE.

