Maoni mbalimbali kuhusu tuzo la Ballon Dor yanazidi kuibuka ulaya huku wachezaji nguli wengine ambao walishastaafu wanazidi kuibua hisia zao.
Baada ya tuzo ya Ballon Dor kupewa Kiungo wa Man City Rodrigo kuna baadhi ya wachezaji waliostafu wanasema sio sawa kwa Real Madrid kufanya tukio la kususia hafla ya kutoa tuzo hizo.
Mshambuliaji wa zamani wa Man City Sergio Kun Aguero anasema haikuwa heshima na busara kwa Madrid kukataa kwenda Paris Ufaransa kwa tuzo hizo, Aguero anasema haikuwa lazima Ballon Dor ya wanaume mshindi atoke Real Madrid kwani tuzo hilo ni la mchezaji yoyote na wala sio lazima awe mchezaji wa klabu fulani.
Clarence Seedorf, mchezaji wa zamani wa AC Milan, Real Madrid na Ajax anasema kiukweli Kulingana na takwimu Vinicius Jr wa Real alistahili kushinda tuzo hiyo lakini haikuwa sawa wa Madrid kususia hafla ya kutoa tuzo hizo.

