ACADEMY ZA SOKA KUJENGWA KOTE NCHINI

Huenda soka la Kenya likaimarika baada ya uamuzi wa wizara ya michezo nchini kutangaza kuwa inalenga kujenga vyuo vya mafunzo na malezi ya soka ukipenda Soccer academy kote nchini.

Kulingana na Waziri wa michezo Kipchumba Murkomen ni kuwa Academy takriban 290 zinatarajiwa kujengwa ndani ya kipindi cha miaka minne ijayo na zitajengwa kwa ushirikiano na shule katika ngazi za maeneo bunge nchini.

Murkomen aliyasema hayo katika hafla ya kutuza wachezaji wa Harambe rising stars ambao ilirejea kutoka kwa mashindano ya Cecafa ambayo yalitumika kwenye kufuzu AFCON U20 mwaka ujao

Wachezaji wa Rising Stars waliofuzu kwa mashindano ya U20 AFCON ya mwaka ujao wanasema wamefurahishwa na tukio hilo kwani ndio timu ya kwanza katika kiwango hicho nchini kuwahi kufuzu kutoka hapa nchini.