Mchezaji wa zamani wa kikosi cha Harambee stars mwite Tyron Otieno amebainisha kuwa kuna uozo mkubwa katika shirikisho la soka la Kenya haswa kwenye masuala ya malipo.
Kulingana na Tyron kwenye ukanda unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni kuwa shirikisho la soka chini ya Nick mwendwa limekuwa likichelewesha malipo ya wachezaji pamoja na kuwashughulikia pindi wanapooumia wakilijukumikia taifa.
”Pale kwenye FKF kuna shinda nyingi, unaweza pata mchezaji anacheza anacheza mechi vizuri lakini malipo yanakuja baada yasiku sitini, ukiumia wanasema wewe ni mzee. Hapa wanasubiri ukufe halafu walete bendera ya kenya kwenye jeneza lako kuashiria ulileta mchango kwa taifa.”
Kwa sasa mchezaji huyo wa zamani wa Harambee stars ameibukia kuuza samaki mtaani Gikombaa baada ya kuachana na soka
”Kwa sasa mimi niko tu katika maeneo haya kuuza samaki, huko niliacha” Alisema Otieno.

