GALATASARAY YALENGA KUMNASA KABISA OSEMHEN

Klabu ya Galatasaray ya Uturuki inalenga  kuufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen kutoka Napoli kuwa wa kudumu, huku Chelsea wakiendelea kumsaka. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atagharimu pauni milioni 68 mwezi Januari au pauni milioni 63 msimu ujao.

Awali mchezaji huyo alifeli kwenye dili la kuihamia klabu ya Chelsea kutokana na mazungumzo kukosa kuafikiwa siku ya mwisho. Tatizo kubwa lilikuwa ni mshahara mkubwa wa mchezaji huyo bora wa Afrika.

Hata hivyo kulikuwa na tetesi za yeye kupewa mshahara anaotaka wa kumpeleka katika ligi ya Saudi Arabia Pro League.

Victor Osemhen amekuwa mchezaji muhimu katika klabu ya Napoli katika msimu ya hivi punde akiisaidia kushinda kombe la Seria A baada ya kipindi cha muda mrefu.