OLUNGA ASEMA HARAMBEE STARS IKO VIZURI

Nahodha wa timu ya taifa Michael Olunga anaimani na kikosi cha Harambee stars cha sasa akisema hakina majeruhi wengi jambo ambalo linawafanya kuamini kuwa licha ya kwamba wwtamenyana na mpinzani mgumu Cameroon wataibuka na matokeo mazuri.

Harambe stars wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Lions wa Cameroon katika mechi ya kuwania tikiti ya kufuzu kwa AFCON 2025 mechi ambayo itachezwa hiyo kesho.

”Kwa sasa kikosi kiko vizuri hata wale waliokuwa na majeraha naona wengi wamerudi. Mimi pia nimeponapona na niko tayari kwa mapambano. Tuko na mechi mbili zote dhidi ya Cameroon na tuko na matumaini huenda tukapata matokeo mazuri.” Olunga alisema

Olunga ameomba mashabiki wa Kenya kuipa sapoti timu hiyo ili wapate morali wa kuandikisha matokeo mazuri katika mechi hizo mbili dhidi ya Cameroon.

”Tunaomba wakenya watupe sapoti ya kutosha manake tunawahitaji sana kipindi hiki ambacho tuko na mpinzani mgumu.” Olunga aliongeza