FKF YAZINDUA KAMATI YA UCHAGUZI MKUU

Shirikisho la soka la fkf nchini kenya jana lilizindua bodi ya watu watano watakao simamia uchaguzi mkuu ujao wa kitaifa katika shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika mwezi disemba mwaka huu.

Bodi hiyo ilichaguliwa na wawakilishi wa vilabu katika kikao maalumu kilichofanyika tarehe 24 mwezi Agosti.

Anayeongoza bodi hiyo ya watu watanoni hesbone owila ambaye ameahidi kuandaa uchaguzi wa haki na huru mwaka huu.

Viongozi wengine katika bodi hiyo ni pamoja na rais wa chama cha waandishi wa habari za michezo sports cha Kenya James waindi, Alfred Nganga, Dan Mule na Merciline Sande ambaye atahudumu kama katibu mkuu.