TOM LANGO KUPIGWA BREKI NA WADAU WA SOKA

Wadau wa soka  la mashinani katika zone C ya eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wanapanga kuelekea mahakamani na kusitisha mipango na azma ya mwenyekiti wa shirikihso la soka katika eneo hilo Tom Lango kuwania kiti cha uenyekiti wa shirikihso la fkf wa kaunti ya kilifi.

Wakiongozwa na Joshua Kazungu Chadi ambaye ni Kocha Gabba United klabu inaoshiriki ligi ya kaunti ya Kilifi ameambia Tama La Spoti kuwa wameshtushwa na taarifa za Lango kutaka kuachana na ligi hiyo kwa kile wanachotaja kuwa bado kuna ahadi ambazo mwenye kiti huyo hajatimizia vilabu vya Malindi.

Kati ya ahadi hizo ni pamoja na  Lango kuambia vilabu vya Malindi kuwa angeleta vilabu vya Nairobi ambavyo soka lao limekuwa kuja mashinani na kutangamana na wachezaji wa Malindi.

Hata hivyo hadi sasa Lango hajajibu chochote kuhusiana na madai hayo huku akizidisha kujinadi kwa vilabu mbalimbali Kilifi akisaka uungaji mkono, mitandao ya WhatsApp na facebook ndio anayotumia sana kwa sasa.