BANDARI YOUTH IMEPANDA ‘DIV 2’

Kocha mkuu wa klabu ya Bandari Youth Alex Shikanga, mkufunzi 2a klabu hiyo ambayo wiki jana ilifuzu kwa mashindano ya kitaifa ya daraja la pili amewapongeza vijana wake kwa kupambania nafasi hiyo katika mini league ya mkoa wa pwani

Shikanga akizungumza na Tama La SPOTI anasema kujituma kwa wachezaji wake ndio kuliwafanya wafuzu licha wa ugumu wa mini league.

”Tulijikakamua vilivyo ili kupata matokeo haya na hatumaye kupanda. Hii imeletwa na kujiamini tangia mwanzoni na wachezaji wetu wazuri. Bandari Youth azma yetu ni kukuza talanta za wachezaji zionekane kitaifa na tumefanikiwa pakubwa kufikia sasa.” Shikanga alizungumza

Shikanga amethibitisha kuwa lengo la Bandari Youth nikukuza talanta na ndio jambo ambalo limevutia mafanikio makubwa hadi sasa wamevuka daraja