Mwenyekiti wa FKF katika eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi Tom Lango ametangaza azma yake ya kupigania kiti cha uenyekiti wa shirikihso la soka la fkf kusimamia kaunti nzima ya kilifi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kusimama mwaka huu.
Akizungumza na Lulu FM kupitia njia ya simu Lango amesema analenga kuleta sura mpya ya soka la kaunti ya Kilifi tofauti na uongozi wa sasa wa Dickson Angore. Amesema analenga kuanza kuzawadi timu na wachezaji bora kila msimu tofauti na inavyofanyika kwa sasa.
Hata hivyo Lango anatarajiwa kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa fkf kaunti ya Kilifi Dickson Angore. Tom ametaja kuwa amesalitiwa na Angore ambaye miaka minne ilopita alimuahidi kumuunga mkono katika azma yake ila sasa Angore naye kulingana naLango ametangaza kusimama. Lango ameahidi kukabiliana naye katika kipute hicho.
Kulingana na taarifa ni kuwa uchaguzi huo ambao tarehe yake rasi haijatangazwa utafanyika kabla ya tarehe 15 disemba mwaka huu huku wagombea wa vyeo mashinani na kitaifa wakizidi kujinadi.

