Mkufunzi mpya wa klabu ya Young Bulls Ali Mwachaunga analenga kuzidi kukiimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao kwa kuzidi kuandaa mechi za kirafiki ili kujinoa zaidi.
Mwachaunga analenga kuongoza Young Bulls kwenye mechi ya pili ya kirafiki tangu kuchukua majukumu katika klabu hiyo msimu hii na wikendi hii Jumamosi watachuana na Kenya Navy katika uwanja wa Alaskan.
Mechi ya kwanza Young Bulls ilicheza dhidi ya Magarini Combined wikendi ilopita na kusajili ushindi wa mabao 2-0
Mwachaunga ni kocha wa zamani wa klabu ya SS ASSAD ya kaunti ya kwale inayoshiriki ligi ya NSL na alihusika kufikisha klabu hiyo katika daraja hilo la kitaifa.
Young bUlls Mwachaunga amesaini mkataba wa mwaka mmoja na lengo lake ni kuipandisha daraja klabu hiyo hadi ligi ya NSL

