RONALDO ALENGA MABAO 1000

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo alifungua ukurasa wake mpya wa kufikisha mabao elfu moja kabla ya kustafu soka la kulipwa.

Jana Mshambuliaji huyo anayecheza soka la mpunga mrefu huko Saudi Arabia na klabu ya Al Nassir alifunga bao lake la 901 akiwa na timu yake ya Ureno kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Scotland.

Ronaldo ambaye kwa sasa ndiye mchezaji mwenye mabao mengi ulimwengu baada ya kufikisha mabao 900 wiki jana alitangaza kuwa analenga kufikisha mabao 1000 kabla kustafu kwake soka la ushindani.

Ronaldo amenukuliwa akisema kuwa analenga kuzidi kulitikisa soka la dunia licha ya umri wake mkubwa, amedokeza kuwa huenda akashiriki katika kombe la dunia makala ya 2026.